IFM YATAKIWA KUBUNI NA KUBORESHA MITAALA YAO

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ametoa wito kwa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuendeleza juhudi za kubuni na kuboresha mitaala ili kutoa mafunzo kwa viwango vya kimataifa kwa vijana wa kitanzania. Ametoa rai hiyo jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya Arobaini na Tisa (49) ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha. Mhe. Chande alisema mifumo ya elimu imeendelea kubadilika kutokana na mazingira yaliyopo na mabadiliko hayo hayazuiliki, kwa kuwa mambo mapya yanaibuka kila wakati.