IFC YAISHAURI TANZANIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA PPP

Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (International Finance Cooperation – IFC) imeishauri Tanzania kuchagua miradi mikubwa michache, endelevu na inayovutia uwekezaji katika Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) ili kufungua biashara na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaaban kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi hiyo, Bi. Amena Arif, kando ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Jijini Nairobi nchini Kenya.