ELIMU YA FEDHA YAWAINGIA WANANCHI WA IRAMBA
Wizara ya Fedha imepongezwa kwa kuendelea kutoa elimu ya fedha vijijini ambako wananchi wengi wameathirika kiuchumi kutokana na matumizi mabaya ya fedha kutokana na kukosa elimu kuhusu matumizi ya fedha, kuweka akiba na kukopa bila kutekeleza malengo yaliyokusudiwa.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, alipoungana na wajasiriamali na Wananchi wa Iramba mkoani Singida katika ukumbi mpya wa mikutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wialayani Iramba, kupata mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -TAMISEMI.