ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WALIMU BIHARAMULO
Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha inayotoa hudumaa ya elimu ya huduma ndogo za fedha imewafikia walimu wa Shule za Msingi, Sekondari na Wakuu wa Idara za Elimu na kuwaelimisha kuhusu masuala ya fedha ikiwemo kujiepusha na mikopo isiyo salama.
Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa St. Clara, wilayani Biharamulo mkoani Kagera, ambapo zaidi ya walimu 650 wameshiriki semina hiyo ambapo walipata fursa ya kujifunza mada zaidi ya nne ikiwemo, kujiwekea akiba, mikopo, uwekezaji, na usimamizi wa fedha binafsi.