ELIMU YA FEDHA YAFIKA MKOA WA KAGERA

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima, amewataka watoa huduma za Fedha kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania wakati wa kutoa huduma za fedha kwa wananchi. Agizo hilo amelitoa alipokutana na Timu ya wataalamu ya Wizara ya Fedha ambao wamefika mkoani Kagera kwa ajili ya kutoa elimu ya huduma za fedha kwa wananchi katika makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wajasiriamali na wanafunzi.