ELIMU YA FEDHA KUWAFIKIA WANANCHI WOTE IFIKAPO MWAKA 2O26
Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi yote ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2930.
Hadi sasa Wizara ya Fedha imetoa elimu ya fedha katika mikoa 15, ikiwemo mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara.