EADB YAONGEZA FURSA ZA UWEKEZAJI NA UFADHILI NCHINI TANZANIA.

Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imeendelea kuongeza fursa za uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu katika nchi wanachama. Mchango huo umeendelea kuonekana kupitia ufadhili na uwekezaji wa Benki katika sekta mbalimbali, ikiwemo miundombinu, makazi, huduma za kifedha, viwanda na huduma za kijamii.