DPP AKABIDHI MALI ZA BILIONI 4.4 ZILIZOTAIFISHWA KWA SERIKALI

Ofisi ya Mkurungenzi wa Mashtaka nchini imekabidhi mali mbalimbali 8188 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4 zilizotaifishwa na Serikali kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. Makabidhiano ya mali hizo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Sylvester Mwakitalu.