DKT. NCHEMBA ZIARANI OMAN APONGEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Muscat- Oman na wadau wengine katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi. Amempongeza Mhe. Balozi Fatma Rajab kwa kazi kubwa na njema ya kueneza diplomasia ya kiuchumi nchini humo kwa mafanikio makubwa.