DKT. NCHEMBA: WADAU WAWEKEZE KWENYE SEKTA ZA UZALISHAJI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa rai kwa wadau wa maendeleo nchini likiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kuiunga mkono Serikali katika uelekeo wake wa kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji ili kuondoa umaskini kwa wananchi.
Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Shigeki Komatsubara ambapo walijadili kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Serikali na Shirika hilo.