DKT. NCHEMBA: TANZANIA IMEPIGA HATUA KIUCHUMI NA KIDEMOKRASIA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amelihakikishia Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora, demokrasia na usimamizi imara wa uchumi wa nchi.
Dkt. Nchemba amesema hayo alipoongoza ujumbe wa Ta
nzani, kukutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Shirika hilo, ukiongozwa na Makamu wake wa Rais Mhe. Alicia Mandaville, Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pande hizo mbili zilijadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kusaidia mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kutatua vikwazo vya ukuaji uchumi, kupitia ruzuku itakayotolewa na Shirika hilo.