DKT NCHEMBA AZINDUA MFUMO WA KIELETRONIKI WA FORODHA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaongoza Mawaziri wa Nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software), utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kiforodha. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.