DKT. NCHEMBA AWASISITIZA WATUMISHI KUSIMAMIA UCHUMI.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaagiza viongozi na watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu ili kuendelea kusimamia uchumi wa nchi. Ametoa agizo hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba, wakati wa Kikao cha watumishi wa Wizara hiyo ambacho kinatoa fursa kwa watumishi kukutana kwa pamoja, kukumbushana na kubadilishana uzoefu, taarifa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Serikali kwa ujumla.