DKT. NCHEMBA AWASILISHA MUSWADA WA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA WA MWAKA 2023
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amewasilisha muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023 wenye dhumuni la kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi.
Akiwasilisha muswada huo bungeni jijini Dodoma Dkt. Nchemba, alisema kuwa muswada huo utaimarisha mazingira ya ununuzi na ugavi kwa taasisi na mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara na kupunguza muda katika hatua na michakato ya zabuni.