DKT. NCHEMBA AWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA MWONGOZO WA BAJETI 2024/25
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi tilioni 47.424 katika mwaka 2024/2025.
Dkt. Nchemba alisema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25.
Alisema kuwa makusanyo hayo yatatokana na vyanzo mbalimbali yakiwemo mapato ya ndani, michango kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na mikopo.