DKT. NCHEMBA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA ITALIA ILI KUKUZA AJIRA NA UCHUMI WA NCHI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa wawekezaji kutoka nchini Italia kutumia mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kuwekeza mitaji yao katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kukuza uchumi wa pande hizo mbili.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.