DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA FEDHA WA KONGO KUHUSU UJENZI WA RELI YA KISASA-SGR

Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Nicolas Kazadi, kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza nchini Tanzania hadi Gitega nchini Burundi kupitia Musongati kwenye machimbo ya madini na kipande kingine cha reli kinachokusudiwa kufika KINDU nchini DRC kupitia Uvira kwenye mpaka wa Burundi na DRC. Mazunguzo hayo yamefanyika mjini Kinshara, Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kando ya mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa jopo la mapitio ya uchumi mpana katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).