DKT. NCHEMBA ATETA NA WAWEKEZAJI NCHINI UINGEREZA
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Royal Africa Society, Dkt. Nicholas Westcott (kushoto) wakati wa Mkutano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Uingereza jijini London. Mkutano huo ulilenga kuwashawishi wafanyabiashara hao kuwekeza nchini Tanzania, Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu-Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil na Balozi wa Tanzania-Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro.