DKT. NCHEMBA ATETA NA VIONGOZI WA MIKOA TANZANIA BARA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kusimamia ipasavyo shughuli za biashara katika maeneo yao na kuwazuia watendaji wa Taasisi za Serikali kufunga biashara za watu kunapojitokeza mizozo ya ukusanyaji kodi, tozo na mambo mengine kwa sababu hatua za kufunga biashara na ofisi hizo ina athari kubwa kiuchumi na ajira za watu Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo Katika Shule ya Uongozi ya Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani, wakati akitoa mada kuhusu hali ya uchumi wa nchi na utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, ulioandaliwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI.