DKT. NCHEMBA ATETA NA MAWAZIRI WENZAKE UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika mkutano na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya viwanda na Biashara, uwekezaji, na masuala ya kodi. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na wataalamu waandamizi kutoka Wizara hizo.