DKT. NCHEMBA ATETA NA MABALOZI WA CANADA NA JAPAN NCHINI

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wawili, Balozi wa Canada na Japan kwa nyakati tofauti ambapo walizungumzia ushirikiano kati ya nchi hizo katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, na sekta binafsi ili kukuza uchumi. Mazungumzo hayo yamefanya kwenye Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.