DKT NCHEMBA ATETA NA BALOZI WA CHINA KUHUSU USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA MRADI WA SGR
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.