DKT. NCHEMBA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania pamoja na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ambako anafanya ziara ya kikazi. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, Mwambata Fedha, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bi. Anath Lwenduru, na kulia kwake ni Balozi wa Tanzania- Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine.