DKT. NCHEMBA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Uganda, Mhe Meja Jenerali Paul Simuli, alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Kampala nchini Uganda, baada ya kuhitimisha Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki (EADB), ambapo aliwapongeza Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo na watumishi wa Ubalozi huo kwa kazi nzuri wanayofanya.