DKT NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA MAGAVANA WA BENKI YA DUNIA JIJINI WASHINGTON D.C NCHINI MAREKANI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika (African Caucus - WB) uliomshirikisha Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Dkt. Nchemba, anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.