DKT. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA IDA21 JIJINI NAIROBI-KENYA
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), ameshiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.