DKT. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA 50 WA BODI YA WADHAMINI YA BENKI YA EADB

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Ng’ongo John Mbadi, wakati walipokutana katika Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), uliofanyika tarehe 13 Machi 2025, katika Hoteli ya Serena, jijini Kampala-Uganda. Mkutano huo uliwashirikisha Wadhamini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono.