DKT. NCHEMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA MAWAZIRI WA FEDHA NA UWEKEZAJI WA SADC

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Jopo la Mapitio ya Uchumi Jumla wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam, ambapo mawaziri hao wamejadiliana masuala ya utangamano wa Jumuiya hiyo, katika nchi wanachama pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kikanda wa SADC utakaotumika kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango na miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo.