DKT. NCHEMBA AONGOZA MKUTANO WA 16 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati), akiongoza Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) na mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudani Kusini, Mhe. Mhandisi Awow Daniel Chuang Deng, ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Baraza hilo, uliofanyika jijini Arusha, nchini Tanzania, ambapo Mawaziri hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo Wasilisho la nchi Wanachama kuhusu Miongozo ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 na Kaulimbiu za bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Forodha, Biashara na Fedha, Bi. Annette Ssemuwemba Mutaawe.