DKT. NCHEMBA AMUAHIDI USHIRIKIANO KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA FEDHA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amemhakikishia Katibu Mkuu mpya na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El -Maamry Mwamba kwamba Wafanyakazi wa Wizara hiyo watampa ushirikiano wa karibu ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia uchumi wa nchi kwa mafanikio. Dkt. Nchemba alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha Dkt. Mwamba katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Chamwino, Dodoma.