DKT. NCHEMBA ALISHAURI BARAZA LA MAWAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI WA EAC KUTAFITI VIKWAZO VYA KUFIKIA MALENGO YA KIUCHUMI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu lameck Nchemba, amezishauri nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya utafiti ili kufahamu sababu za nchi hizo kushindwa kufikia vigezo mtangamano wa uchumi mpana ambavyo ni moja kati ya vigezo vya nchi hizo kufanikisha itifaki ya Umoja wa Sarafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2031. Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo wakati wa mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo ulipokea na kujadili taarifa mbalimbali za mkutano uliopita wa Baraza hilo.