DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA MOODY'S

Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na kuzifanyia tathimini nchi mbalimbali ili kujua uwezo wake wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya Kimataifa, Moody’s, imetua nchini kwa ajili ya kufanya tathimini hiyo Tanzania. Akizungumza wakati akiikaribisha timu ya wataalam kutoka Taasisi hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa tathimini hiyo ni fursa kwa Tanzania kuweza kuyafikia Masoko ya fedha ya Kimataifa yatakayoiwezesha nchi kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.