DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA LAAC KUTOKA BUNGE LA ZAMBIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kutoka Bunge la Zambia wakiongozwa na Mhe. Darious Mulunda ambao wako katika ziara nchini, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.