DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA ORASCOM
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, Bw. Ashraf Roushdi, ambapo Kampuni hiyo imeonesha nia yake ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya Mkutano huo uliofanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko, pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha.