DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the World Bank Group – for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Floribert Ngaruko, Ofisi ya Hazina Ndogo, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha pia Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, Naibu Katibu Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine wa Wizara ya Fedha.