DKT. NCHEMBA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA CGP JEREMIA KATUNGU
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye amefika ofisini kwake kujitambulisha, akiwa ameambatana na Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya namna ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa majukumu ya Jeshi hilo yanatekelezwa kwa ufanisi.