DKT. NCHEMBA AITA WAWEKEZAJI KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa wito kwa wawekezaji wa kimataifa pamoja na wazawa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania katika sekta mbalimbali. Dkt. Nchemba ametoa wito huo mjini Washington D.C, Marekani, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi anayesimamia masuala ya masoko ya mitaji, maendeleo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Sarvesh Suri, ambapo Dkt. Nchemba anaongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).