DKT. NCHEMBA AISHUKURU IMF KWA KUSAIDIA MAENDELEO YA NCHI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefungua vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchachua na kutengemaza uchumi kupitia sekta za uzalishaji. Alitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika hilo kwa kutoa fedha zinazotumika kutekeleza miradi inayosaidia kuchochea maendeleo ya wananchi, kukuza uchumi jumuishi na kuiwezesha nchi kuhimili misukosuko ya kiuchumi inayoikabili dunia.