DKT. NCHEMBA AISHAURI ANGLO GOLD ASHANTI KUIUZIA DHAHABU BENKI KUU YA TANZANIA

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameushauri uongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine-GGM), kuanza kuiuzia Serikali dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania ili kuiwezesha Serikali kuhifadhi dhahabu kama akiba ya fedha za kigeni. Dkt. Nchemba ametoa ushauri huo Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni hiyo, Bi. Gillian Doran, ambapo wamejadili masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Serikali.