DKT. NCHEMBA AIOMBA BENKI YA DUNIA KUISAIDIA SERIKALI KUBABILIANA NA UPUNGUFU WA DOLA ZA MAREKANI

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameiambia Benki ya Dunia kwamba Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwezesha upatikanaji wa fedha za kigeni kupitia uwekezaji wa mitaji kutoka ndani na nje ya nchi. Dkt. Nchemba, amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bw. Hassan Zaman, katika Ofisi za Hazina Ndogo Jijini Dar es Salaam.