DKT. NCHEMBA AIHAKIKISHIA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUBORESHA MIFUMO Ya KODI

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi. Dkt. Nchemba ameyasema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot.