DKT. NCHEMBA AIAGIZA PPRA KUUNGANISHA MFUMO WA GIMIS NA NeST

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhakikisha inaunganisha Mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) na Mfumo Jumuishi wa Kielektroniki katika Utoaji wa Huduma za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GIMIS) ili kurahisisha mchakato wa ununuzi Serikalini. Waziri Nchemba akitoa maelekezo hayo wakati akizindua wa Mfumo Jumuishi wa Kielektroniki katika Utoaji wa Huduma za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini ujulikanao kama GIMIS (GPSA Intergrated Management Informationm System), uliofanyika katika katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina Jijini Dodoma.