DKT NCHEMBA AHIMIZA UIMARISHAJI WA NISHATI NCHI ZA AFRIKA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amezihimiza nchi za Afrika kwa kushirikiana na Taasisi za Fedha Duniani pamoja na Sekta Binafsi, kuhakikisha kuwa zinawekeza kwenye uzalishaji wa nishati ya uhakika na yenye gharama nafuu ili kutimiza malengo ya kujiimarisha kiuchumi, kuchochea uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa na huduma na kukuza ajira.