DKT. MWINYI ATOA NENO KUELEKEA MKUTANO WA BENKI YA DUNIA - ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya kufanya mahojiano maalumu kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid-Term Review) utakaofanyika Zanzibar, kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukiwashirikisha wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa takribani 100 duniani. Katika mahojiano hayo, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi, amewakaribisha washiriki wa mkutano huo nchini Tanzania hususan, katika Visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar), ili kushuhudia Maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii yaliyofikiwa kupitia mikopo nafuu na misaada kupitia Benki ya Dunia na amewataka wananchi kuchangamkia fursa za ugeni huo katika Sekta mbalimbali ikiwemo utalii.