DKT. MWIGULU NCHEMBA ATETA NA KAMISHNA WA BIASHARA KANDA YA AFRIKA WA UINGEREZA

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Tanzania amelishauri Shirika la Kimataifa la Uwekezaji la Uingereza (British International Investment- (BII), kuongeza kiwango cha uwekezaji nchini Tanzania ili kukuza biashara Dkt. Nchemba ametoa wito huo Jijini London, nchini Uingereza, alipoongoza Ujumbe wa Tanzania uliokutana na Menejimenti ya Shirika hilo, ambalo limewekeza katika baadhi ya miradi nchini hapa.