DKT. MWIGULU NCHEMBA ANA KWA ANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA AUSTRIA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewahimiza wawekezaji kutoka Austria na Ujerumani, kuharakisha mchakato wa kuwekeza katika sekta ya ujenzi wa makazi ya kisasa na ya gharama nafuu ili kutatua changamoto ya makazi hususan kwenye taasisi za umma hapa nchini. Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Austria na ujerumani, ukiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa 10 wa Austria, Dkt. Alfred Gusenbauer, jijini Dar es Salaam.