DKT. MWIGULU AWATAKA VIJANA WAHITIMU KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA MAENDELEO

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazojitokeza ndani na nje ya nchi. Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Fedha katika Mahafali ya 37 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini duru ya pili katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya ziwa - Mwanza, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, aliwataka wahitimu hao kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na mazingira yanayotengenezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.