DKT. MWAMBA ATOA MAELEKEZO KUHUSU UHUISHAJI WA MIPANGO MIKAKATI KWA KUENDANA NA DIRA 2050
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba amewaagiza Wataalam wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali kuhuisha mipango mikakati ya mafungu yao (institutional strategic plans) kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Miaka 25 (Vision 2050), Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV) na Mwongozo wa Uandaaji wa Mipango Mikakati unaotolewa na Tume ya Mipango ili kuhakikisha vipaumbele vya taifa vinatekelezwa ipasavyo.
Ametoa agizo hilo jijini Dodoma, katika kikao cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, kufanya Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2024/25 na Maandalizi ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2025/26.