DKT. MWAMBA ATETA NA UJUMBE KUTOKA EU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans, alieongoza Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya baada ya kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024.