DKT. MWAMBA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA KITAIFA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, Dkt. Natu El Maamry Mwamba ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) jijini Dodoma ambapo wajumbe walipokea na kujadili hatua iliyofikiwa ya utejkelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Tasisi ya TradeMark Africa (TMA) pamoja na masuala mbalimbali ya kibiashara yenye lengo la kukuza uchumi wa nchi.